Usiku wa May 22 umefanyika mchakato wa utoaji Tuzo za watu ambao ulifanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Hotel jijini Dar es salaam . Hii ni baada ya mchakato huu kuchukuwa muda mrefu kwa wananchi kuwapigia kura wale walikuwa ndio Nominees katika Tuzo hizo kwa takribani muda wa wiki kadhaa zilizopita . Tuzo za watu zinaadhimishwa na mtandao wa Bongo 5 na majaji wake huwa wananchi wenyewe ambao ndo wanapendekeza na kupiga kura mpaka kupatikana mshindi . Baada ya utoaji Tuzo kufanyika #Alikiba aliibuka msanii bora wa kiume anayependwa zaidi Tanzania aliuwa na mastaa wengine katika nafasi zao.............
Vipengele vya kushindania vilikuwa takribani kumi na mbili (12) ambapo ni pamoja na #Muigizaji bora wa filamu wa kike #Muigizaji bora wa filamu wa kiume #Muongozaji bora wa filamu #Kipindi cha runinga #Kipindi cha redio #Mtangazaji wa runinga anaye pendwa #Mtangazaji wa redio #Msanii wa kiume anaye pendwa #Video bora #Msanii bora wa kike #Muongozaji wa Video #Tovuti bora . Baada ya mchakato mzima wa upigaji kura kufanyika wafuatao ndio waliibuka washindi katika nafasi zao................
# Muongozaji bora wa filamu

Vient kigosi a.k.a Ray
#Muigizaji bora wa kike

Wema sepetu
#Muigizaji bora wa kiume

Hemed suleiman
#Kipindi bora cha runinga

Mkasi - cha Salama Jabiri
#Kipindi bora cha redio
Papaso TBC fm cha DJaro Arungu
#Mtangazaji wa runinga anayependwa
Salim kikeke - Hidaya ya kiswahili Bbc
#Mtangazaji wa redio anayependwa

DJaro Arungu - Papaso TBC fm
#Msanii bora wa kiume anayependwa

Alikiba - hitmaker wa #Chekecha cheketua
#Msanii bora wa kike anayependwa
Lady Jay Dee - hitmaker wa #Forever
#Video bora inayopendwa

Nani kama mama - Christian bella ft Ommy dimpoz
#Muongozaji bora
Hans cana
#Tovuti bora
Mllardayo.com - Millard ayo
No comments:
Post a Comment