Social Icons

Pages

Saturday, 16 May 2015

Diamond platnumz kukutana na balozi wa Tanzania nchini Uingereza


















Raisi wa wasafi Diamond platnumz a.k.a Mond bin Laden kama anavyojiita yeye mwenyewe amefanikiwa kukutana na balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh.Peter Kallaghe katika tour yake ya show nchini humo ambayo ilianza siku ya alhamisi May14 nchini Uingereza.Kwakupitia ukurasa wake wa instagram Diamond platnumz amepost picha na kuandika "Shukrani sana Mh.balozi kwakutukarimu vizuri ubalozini jana Yesterday at our Tanzania Uk Embassy".

















Platnumz yupo nchini Uingereza kwaajili ya show yake ya Diamond Are Forever ambayo inatarajiwa kufanyika usiku wa leo May16 nchini humo .Show hiyo ilianza kupewa shamra shamra kwa muda mrefu kwakupitia mitandao yake ya kijamii ambapo ameahidi kuwa itakuwa ni ya kihistoria kutokea.

No comments:

Post a Comment

 
Blogger Templates